Tuesday, 3 December 2019

Samatta anaenda Uingereza

Mbwana Samatta abadilisha Wakala
2 hours ago


Nyota wa klabu ya KRC Genk, Mbwana Samatta  ameondoka katika kampuni ya uwakala ya First For Players na kujiunga na Spocs Consultant inayomsimamia Mohamed Salah wa Liverpool.

Samatta anakuwa mchezaji wa pili mwenye thamani ya juu kwa wanaosimamiwa na kampuni hiyo baada ya Mo Salah.

Samatta ambaye ni mchezaji namba mbili kwa thamani katika list ya wachezaji zaidi ya 100 wanaosimamiwa na Spocs Consultant, aliingia mkataba na First For Players December 22 2018 lakini ameamua kubadilisha wakala kwa sasa ili aweze kutimiza ndoto zake za kucheza ligi kuu ya England.


Saturday, 30 November 2019

Breaking: Rasmi Kocha Aussems Afungasha Virago Simba Sc
53 minutes ago

Kocha wa Simba Mbelgiji, Patrick Aussems, kupitia akaunti yake rasmi ya Instagram leo Novemba 30, 2019 amethibitisha kuwa Bodi ya Wakurugenzi ya klabu ya Simba, kupitia kwa Mtendaji mkuu wa timu hiyo, Senzo Mazingiza, imemtaarifu kwamba, kuanza sasa, yeye sio kocha mkuu wa timu ya Simba SC.

Thursday, 28 November 2019

Nafasi mpya za ajira Tanesco

Nafasi 62 za Kazi TANESCO | Wanahitajika watu wa Customer Care
5 hours ago
Nafasi 62 za Kazi TANESCO | Wanahitajika watu wa Customer  Care 
▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬

👉Mwisho wa Kutuma maombi ni;11/12/2019
👉Elimu ni  Diploma ya Marketing, Public Relations au  Business Administration 
👉Mwenye Elimu Kidogo ya Computer atapewa Kipaumbele

👉Uzoefu ni Mwaka mmoja
▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬ 

==>>Kujua namna ya kutuma maombi <<INGIA HAPA>>

Kagere atajwa kuwania mchezaji bora wa afrika

Caf Yampaisha Kagere Tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika
2 hours ago

ZIKIWA zimepita siku chache tangu Shirikisho la Soka Afrika (CAF), kumtangaza mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere kuwa miongoni mwa wachezaji wanaowania Tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika kwa wale wanaocheza ligi ya ndani, sasa mchezaji huyo si wa mchezomchezo baada ya wakala wake kusema anayemhitaji sasa atoe bilioni 1.5.



Kagere amepata nafasi hiyo kutokana na kiwango cha juu alichoonyesha msimu uliopita akiwa na kikosi cha Simba katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuiongoza timu hiyo kufika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo lakini pia yeye mwenyewe akishika nafasi ya pili kwa kuzifumania nyavu baada ya kufunga mabao sita.


Wakala wa Kagere, Patrick Gakumba ameliambia Championi Jumatano kuwa kutokana na hali hiyo thamani ya Kagere sasa imeongezeka mara mbili zaidi ya ile aliyokuwa nayo hapo awali. Alisema hapo awali thamani ya

Kagere ilikuwa ni kuanzia dola 300,000 (zaidi ya Sh milioni 685) lakini kwa sasa timu yoyote ambayo itamhitaji itabidi itoe dola 500,000 (zaidi Sh bilioni 1.143).



“Kusema kweli baada ya kusikia kuwa Kagere amechaguliwa kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora Afrika, nilifurahi sana kwani sasa thamani yake imeongezeka ukilinganisha na ilivyokuwa hapo awali, hakika namshukuru sana Mungu.



“Kwa sasa tunaendelea kumuomba Mungu ili aweze kutusaidia Kagere aweze kuibuka mchezaji bora kwa sababu vigezo anavyo, aliibuka mfungaji bora namba mbili katika michuano hiyo ya Ligi ya Mabingwa Afrika. “Ikitokea akaikosa nafasi hiyo basi hata hapa alipofikia ni sehemu nzuri kwani tayari thamani yake imeongezeka siyo tena wa dola 300,000 sasa ni dola 500,000  na kuendelea.”

Thursday, 7 September 2017

CCM yatoa tamko kuhusu lissu kupigwa risasi

CCM Yatoa Tamko Tundu Lissu Kupigwa Risasi
11 hours ago

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia kwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole kimelaani kitendo alichofanyiwa Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu kwa kupigwa risasi leo mchana nyumbani kwake Dodoma.

Taarifa hiyo ya CCM inalaani kitendo hicho cha kikatili na kusema si kitendo cha utu hivyo kimelitaka jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa tukio hilo na kuwachukulia sheria kali wote ambao watapatikana kuhusika katika tukio hilo. 

Rais Magufuli awataka wateule wake wajitumbue wenyewe

Breaking News: Rais Magufuli Amtaka Simbachawene na Wenzake WAJITUMBUE Wenyewe
17 hours ago
Rais Magufuli amewataka viongozi mbalimbali wa serikali ambao wametajwa kwenye ripoti za bunge ya madini ya Almasi na Tanzanite wamepishe nafasi zao ili vyombo vya usalama viweze kufanya kazi yake vizuri kuwachunguza.

Rais Magufuli amesema hayo leo wakati akikabidhiwa ripoti hizo Ikulu jijini Dar es Salaam na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na kusema amesikia baadhi ya viongozi mbalimbali wengine ambao amewateuwa yeye kuwa wameusishwa kwenye wizi huo hivyo amewataka wapishe.

"Wako watu wametajwa tajwa, na wengine mimi ndio nilihusika kuwateua sasa ukishatajwa tajwa, naagiza vyombo vya ulinzi na usalama vifuatilie hili tena kwa haraka.

" Wale ambao wametajwa tajwa kwenye ripoti hii ambao ni wateule wangu, ili vyombo vya usalama viweze kufanya kazi yake vizuri, ni matumaini yangu watakaa pembeni"alisema Rais Magufuli


Katika ripoti hiyo ambayo iliwasilishwa jana mjini Dodoma na leo kukabidhiwa kwa Rais Magufuli na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa iliweza kuwataja baadhi ya viongozi wa serikali ikiwepo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. George Simbachawene, Waziri wa zamani wa Nishati na Madini na Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja pamoja na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.

Jinsi Tundu lissu alivopigwa risasi

Mbunge wa Rombo Asimulia Jinsi Tundu Lissu Alivyopigwa Risasi
10 hours ago
Mbunge wa Rombo, Joseph  Selasini ameeleza jinsi Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu alivyopigwa risasi nyumbani kwake mjini Dodoma.

Selasini amesema kuwa maelezo aliyopata ni kuwa alikuwa akifuatiliwa na  gari tangu anatoka bungeni na dereva wake alilishtukia.                     

Amesema kuwa alivyoona wanamfutilia alipofika nyumbani, dereva alimsihi Lissu asishuke ndani ya gari.                      

"Hao watu walipoona hawashuki walijifanya kuna kitu wanaangalia walivyoona kuna utulivu walisogeza gari lao ambalo ni tinted na kuanza kurusha risasi upande wa Lissu." amesema                     

Selasini amesema, “Risasi zilimpata mguuni, mkononi na tumboni lakini daktari anasema anaendelea vizuri."

Lissu amepigwa risasi leo Alhamisi  na kupelekwa chumba cha upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma.